Urusi iko tayari kuafikiana na Trump kuhusu Ukraine: Putin

KADUSHI MEDIA
By -
0

 

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema yuko tayari kufikia maafikiano kuhusu kusitisha mapigano na Ukraine katika mazungumzo yanayotarajiwa kufanywa na Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, huku vikosi vya Urusi vikiendelea kusogea na kufikia malengo yake katika uwanja wa vita.

Putin, wakati wa kupokea maswali kupitia njia ya runinga ya Taifa katika kipindi cha maswali na majibu cha kila mwaka kutoka kwa raia wa Urusi, amemuambia mwandishi wa chombo cha Marekani kwamba yuko tayari kukutana na Trump, ambae amesema hajaongea nae kwa miaka kadhaa.

Alipoulizwa ni kitu gani angeweza kumpa Trump, Putin alitupilia mbali madai kwamba Urusi iko katika nafasi dhaifu, na kusema kwamba, Urusi imekuwa na nguvu zaidi tangu alivyoamuru vikosi kuingia Ukraine mwaka 2002.

"Siku zote tumekuwa tukiseam kwamba tuko tayari kwa majadiliano na maafikiano," amesema Putin na kuongeza kuwa vikosi vya Urusi vinaendelea kusogea mbele na kufikia malengo ya msingo Ukraine.

"Hivi karibuni, hao Waukraine ambao wanataka kupigana wataisha, kwa maoni yangu, hivi karibuni hakuna atakaebaki kupigana. Tuko tayari, lakini upande wa pili unatakiwa kuwa tayari kwa majadiliano na maafikiano."

Trump, anayejisifu kwa uzoefu wa kutatua migogoro na mwandishi wa kitabu cha mwaka 1987 'Trump: the Art of the Deal', ameapa kumaliza mgogoro huo, bila kutoa taarifa zaidi ya jinsi atakavyofanikisha

Imeripotiwa kwamba mwezi uliopita kwamba Putin alikuwa tayari kwa majadiliano na Trump kuhusu mpango wa kusitisha mapigano na Ukraine, huku akisisitiza Kiev kuachana na malengo yake ya kujiunga na NATO.

Mashambulizi ya Urusi ya mwaka 2022 dhidi ya Ukraine yamesababisha vifo vya maelfu ya watu, huku mamilioni wakikosa makazi na kusababisha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya Moscow na nchi za Magharibi tangu mgogoro wa makombora ya Cuba wa mwaka 1962.

Urusi mwaka huu, imechukua eneo maelfu ya kilomita za mraba za Ukraine mwaka huu, wakichukua kijiji baadda ya kijiji na kuhatarisha miundombinu ya miji ya kimkakati kama vile Pokrovsk, kitovu cha miundombinu ya barabara na reli.

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)