TAKWIMU ZA UKATILI WA KIJINSIA ZAPUNGUA KWA MWANZA

KADUSHI MEDIA
By -
0

 

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limefanikiwa kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia kutoka matukio 1,140 mwaka jana hadi 1,118 mwaka huu sawa na upungufu ya asilimia 22.


Hayo yamebainishwa leo Disemba 10, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafugwa wakati wa  maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Polisi Mabatini jijini humo.


Kupungua kwa matukio hayo kumetokana na jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi kupitia Mtandao wa Polisi wanawake (TPF NET), Dawati la Jinsia na Watoto na Polisi Kata wa kutoa elimu na kuchukua hatua za kisheria kwa watuhumiwa wa masuala ya ukatili.


Maadhimisho hayo huadhimishwa kila mwaka nchini ifikapo Novemba 25 hadi Disemba 10 ikiambatana na siku ya haki za binadamu.


Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ziliasisiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) awamu ya 7 Kofi Annan mwaka 2006 kwa lengo la kutaka dunia itambue kuwa lipo tatizo kubwa la ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ulimwenguni.



Hii ilitokana na kuazimishwa na kituo cha UN cha wanawake kupinga ukatili wa wanawake na wanaharakati wa kisiasa waliouawa Mirabal Sisters mwaka 1960 kutokana na amri ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rafael Trujillo katika Jamhuri ya watu wa Dominica.


Neye mgeni katika hafla hiyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi ameitaka jamii kupaza sauti kwa pamoja kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.


Sambamba na hayo wadau mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo wametaja baadhi ya sababu zinazosababisha uwepo wa ukatili wa kijinsia ikiwemo afya ya akili na kuliomba Jeshi la Polisi kuendelea kukemea na kuchukua hatua za kisheria kwa watuhumiwa wa vitendo hivyo.






Na Pascal Kadushi


Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)