muhimbili_taifa WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA WAGONJWA MUHIMBILI: APONGEZA MENEJIMENTI NA WATOA HUDUMA

KADUSHI MEDIA
By -
0

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Bi. Mary Majaliwa leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuwajulia hali wagonjwa mbalimbali wanaopata matibabu hospitalini hapo.

Akiwa eneo la tiba na magonjwa ya dharura, Mhe. Majaliwa amewapa pole wagonjwa na kuwatakia heri katika matibabu yao na kuipongeza Menejimenti ya MNH pamoja na watoa huduma wote kutokana na kazi kubwa wanayofanya ya kuhudumia wananchi wanaofika hospitalini hapo kupata huduma mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa yeye pamoja na Menejimenti anayoisimamia na wafanyakazi wote wataendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwapa wananchi huduma stahiki zinazokidhi matarajio yao.




Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)