Katibu Tawala Wilaya ya Bariadi ndugu Justine Manko ameongoza kilele cha Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara Halmashauri ya Mji Bariadi huku akisisitiza umoja,uadilifu mshikamano.
Manko ameongoza Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi.
Aidha amewataka wazazi na walezi kuzingatia maadili kwenye makuzi ya watoto na kupinga vitendo vya ukatili.
Mdahalo huo umejumuisha wazee maarufu,viongozi wa dini,kamati ya ulinzi na usalama,vyama vya Siasa,watumishi pamoja wananchi mdahalo umeongozwa na katibu Tawala Wilaya ya Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Bariadi.
“Kauli Mbili:Uongozi Madhubuti Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu”