Maelfu ya raia wa Lebanon walioachwa bila makazi wameanza kurudi makwao huku usitishwaji wa mapigano kati ya Israeli na Hezbollah ukiendelea. Msururu wa magari yaliyobeba vitu binafsi yalikiuka tahadhari iliyotolewa na Lebanon na vikosi vya Israeli vya kuepuka baadhi ya maeneo.
Iwapo usitishaji huo wa mapigamo utaendelea basi utamaliza mapigano ya miezi kadhaa kati ya Israeli na Hezbollah, ambayo yameongezeka kati kati ya mwezi wa September.
Makubaliano hayo ya kutisisha mapigano hayakujumuisha Gaza, ambapo mashambulizi ya Israeli ya kuamkia leo katika shule mbili zilizotumika kama makazi yameua watu 11, wakiwemo watoto wanne, kwa mujibu wa maafisa wa hospitali.
Makubaliano ya Lebanon yanaweza kuleta sahali kwa watu milioni 1.2 waliokosa makazi na maelfu ya Waisraeli waliokimbia makazi yao pembezoni mwa mpaka.