Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Happy Mbuya kutokea jijini Mwanza,Aliyevuma kwa Nyimbo zake mbalimbali kama Vile,Goliati,Nitakusifu,Heri kupendwa na Yesu,Yesu ni Jibu,Nateka baraka kwa Mungu wangu na Vibao vingi ambavyo ameviachilia kupitia Kwenye Channel yake ya Youtube anayomia kwa Majina ya Happy Mbuya Og
Siku za hivi karibuni mwimbaji huyo ametangaza kuja kivingine zaidi katika kuachia kazi zake,Amesema ataendelea kutoa kazi kulingana na Ujumbe atakao pewa na Roho mtakatifu, lengo nikuwafikia watu na sio kibihashara zaidi,
Mambo makubwa atakayoyazingatia nipamboja ya nakutoa nyimbo nzuri zenye viwango vya Ubora zaidi kuanzia katika Uandaji wa Audio (Mziki) pamoja na video,Ingawa kumekuwepo na changamoto nyingi wakati wa Uandaaji lakini havitakua mwaimba kwake alisema mwimbaji huyo
Sasa anaendelea kutamba na wimbo wake wa HUNIACHI,Ambao upo kwenye mitandao mbalimbali kama vile Youtube,na kwenye mitandao mingine,Anatarajia kuja na Video ya wimbo huo ambao unazaidi ya wiki mbili toka autoe,
kuchelewa kwa video ya wimbo huo amesema nikutokana na Maandalizi makubwa ya Ujio wa Video hiyo
Siku za Hivi karibuni mwimbaji huyu,Alisema kupitia kwenye Mahojiano na Kituo cha Jembefm kiapaji chake kilivumbuliwa na Mtumishi wa Mungu Mwl.Christopher Mwakasege,katika moja ya mikutano yake aliyowahi kufanya jijini mwanza,Mwimbaji huyo alijitokeza baada ya kusikia msukumo ndani yake kwa muda mrefu na Mwl.Mwakasege alisema watu wote wenye msukumo wa kumuimbia Mungu ndani yao waje mbele hapa,
Hakusita kwenda mbele nakuombewa tokea pale alianza kumuimbia Mungu mpaka sasa,Zaidi sana tumekuwekea kiungo (link) hapa chini kwenda kusikiliza kazi zake
Moja ya wimbo wake unaoendelea kubamba sehemu mbalimbali pamoja na nikwenye Vituo vya Redio Mwanza na Tanzania kwa Ujumla
Na mwandishi wetu Mwanza