SHABIKI MKONGWE WA PAMBA JIJI,MZEE MANG'OMBE AKABIDHIWA BAISKELI NA MBUNGE WA NYAMAGANA,MH.MABULA

KADUSHI MEDIA
By -
0

 

Shabiki mkongwe wa Timu ya Pamba jiji ya Jijini Mwanza,Mzee Japhet Mang'ombe leo Tarehe 07/08/2024 Amekabiziwa Baiskeli,Jezi ya Timu hiyo ,Bendera ya timu ya Pamba jiji pamoja na tiketi 


Zawadi hizo zimetolewa na  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mh.stanslaus Mabula

Kutokana na majukumu yake,hakuwepo kwenye kukabidhi zawadi hizo,Amewakilishwa na 


Mwenyekiti wa timu ya Pamba jiji,Naibu Meya wa jiji la Mwanza  Mh.Bhiku Kotecha na Katibu tawala wa Wilaya ya Nyamagana,Thomas James Salala pamoja na viongozi mbalimbali wa timu ya Pamba jiji.



Mh.Mabula alitoa ahadi ya kumpatia baiskeli mzee Mang'ombe kwa mchango wake mkubwa wa kuishabikia timu ya Pamba jiji kwa zaidi ya miaka 30,Alitoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya kishiri iliyopo katika jimbo la Nyamagana


Mzee Japhet Mang'ombe akitoa burudani miaka ya 90 wakati timu ya pamba ikishiriki ligi kuu,




Mh.Kotecha amempongeza kwakua na mapenzi ya dhati kwa timu ya pamba jiji toka timu inashuka daraja mpaka sasa ni miaka 23 bado ana mapenzi na timu,

Kwaniaba ya serikali Katibu tawala wa Wilaya ya Nyamagana,Thomas James Salala,wamemtaka mzee Mang'ombe atumie nafasi yake kuendelea kufanya hamasa zaidi kuelekea siku ya Tamasha la Pamba day litakalo fanyika siku ya jumamosi ya tarehe 10/08/2024 katika Uwanja wa Ccm Kirumba 

Kwa Upande wake Mzee Mang'ombe amewahidi kutoa Burudani zaidi pale Uwanjani ataonyesha vituko vyake ambavyo ameviboresha zaidi kuliko alivyokua zamani

Mzee Mang'ombe alijizolea Umarufu mkubwa Nyakati hizo akiwa kijana,Wakati timu ya pamba ikicheza alikua akishangilia kwa aina yake kwa kutumia baiskeli akionyesha umaridadi wake,



Pamoja na hayo alikua akitoa hamasa mtaani watu waende uwanjani kwenda kuishangilia timu ya pamba,alikua akizunguka kwa kutumia baiskeli yake.Amesema

"Watu wengi walijua mzee mang'ombe nimeshakufa lakini sasa nataka niwambie watu waje Uwanjani waone mambo yangu hii sura watu hawataiona hiyo siku"Mzee Mang'ombe


Picha za matukio mbalimbali za Utoaji zawadi wa Baiskeli,Tiketi,Jezi na Bendera ya timu ya Pamba jiji








Na Erick Audax

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)