Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Swalala amezindua tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC lililopo Buhongwa jijini Mwanza.
Swalala amezindua tawi hilo Jumamosi Agosti 03, 2024 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Siku ya Pamba (Pamba Day) itakayofanyika Agosti 10, 2024 katika uwanja wa CCM Kirumba
"Ili Pamba Jiji FC ifanye vizuri, lazima kuiunga mkono kwa kununua tiketi na jezi itakapokuwa inacheza. Pia tujitokeze kwa wingi Pamba Day kuishangilia itakapokuwa inacheza na timu ya Vitalo kutoka Burundi" amesema Swalala
.
.