FAIDA YA KUMNYONYESHA MTOTO MIEZI SITA YA AWALI. EMMA AFISA LISHE

KADUSHI MEDIA
By -
0

 

Afisa lishe Jiji la mwanza Ema Vicent Kilimali amewashauri wanawake kuwanyonyesha watoto wao angalau miaka miwili au zaidi Kwani kuna faida kubwa kwa watoto.


Akizungumza na Jembe Fm Agasti 5, 2024 katika kipindi Cha mchakamchaka na kusisitiza kuwa mtoto anapaswa kunyonya maziwa ya mama kwa miezi sita ya awali pasipo kupewa chakula chochote hadi mtoto atakapofikisha miezi sita.


Pia ameshauri kuwa mtoto atakapofikisha miezi sita ataruhusiwa kupewa na chakula kingine pamoja na maziwa ya mama Kwani kwa muda huo maziwa yatakuwa hayajitoshelezi kwa mtoto.





Aidha ameongeza  kuwa kuna faida kubwa kwa mtoto kupatiwa kwa maziwa ya mama pekee kwani humsaidia mtoto kupata chakula sahihi na kwa kiwango sahihi.


Aidha ameeleza madhara yanayoweza kupatikana kwa wazazi ambao hawanyonyeshi watoto wao ipasavyo Kwani ni gharama lakini pia ni ngumu kwa mtoto kusaga chakula Kwani umri wake unakuwa bado mdogo.


Mtoto anaweza kukua kiakili na pia kimwili kwa kutumia maziwa ya mama Kwani maziwa ya mama yana viini lishe ambavyo vinamsaidia mtoto kuwa na uwiano mzuri wa ukuaji na maendeleo mazuri katika mwili wake.


Na Mary Makanza

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)