Waandamanaji wanaoipinga serikali wamerejea barabarani nchini Kenya kuongeza shinikizo la kumtaka rais ajiuzulu, huku Rais William Ruto akishuhudia kuapishwa kwa baraza la mawaziri lililoundwa upya kwa lengo la kuridhisha za wananchi.
Polisi walirusha mabomu ya machozi na kukamata watu siku ya Jumatano katika mji mkuu, Nairobi, ingawa idadi ya watu walioshiriki katika maandamano ilipungua ikilinganishwa na wiki zilizopita.
Barabara zinazoelekea Ikulu, makazi rasmi ya rais, zilifungwa huku mawaziri wapya 19 walioteuliwa waliapishwa baada ya kuidhinishwa na bunge.
Ruto alitoa nyadhifa nne za baraza la mawaziri kwa upinzani katika katika hatua ya ujumuishaji, zikiwemo wizara za fedha na nishati.
“Wakati huu taifa letu unatutaka tujenge ‘timu moja na wapinzani’ thabiti ili kuipa ajenda yetu ya mabadiliko nafasi bora ya mafanikio,” Ruto alisema kwenye hafla hiyo.
Nchi imekumbwa na maandamano ya mwezi mmoja ambayo yalianza kama maandamano ya amani kupinga nyongeza ya ushuru lakini yamebadilika na kuwa kampeni ya kupinga serikali inayotaka Ruto aondoke.
Takriban watu 50 wamefariki tangu maandamano hayo yaanze mwezi uliopita, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu linaloungwa mkono na serikali.
Katika hotuba yake, Ruto alikiri kwamba maafisa wengi wa umma katika utawala wake "walikosa kufikia kiwango cha kikatiba cha maafisa wa umma".
Aliapa kuanzisha hatua za "kutoza ada ya ziada" dhidi ya maafisa wa umma wanaosababisha upotevu wa rasilimali za umma.