ASEKWA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MBAGALA

KADUSHI MEDIA
By -
0

 

Mtuhumiwa Nurdin Mussa Said miaka 20 mkazi wa Mbande Manispaa ya Temeke Agosti 07,2024 amehukumiwa kwenda Gerezani miaka thelathini baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi mwandazi wa Mahakama ya Wilaya Temeke Mh. John Ngeka amesema kuwa Mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo ambapo umefanikisha kumtia hatia mtuhumiwa huyo kuhusika na kosa la kubaka.

Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa mnamo tarehe 12.06.2023 mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya kumdanganya mwanafunzi huyo na kumpatia zawadi tofauti na kufanikiwa kumbaka.

Na mwandishi wetu Dar

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)