JAMII YATAKIWA KUFANYA KWELI KUHAMIA KATIKA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

KADUSHI MEDIA
By -
0

 

Katika kuhakikisha Jamii inafanya kweli katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amesema mpango wa Serikali ni kuona Jamii inafanya kweli kwa kuhama kutoka kwenye Nishati isiyokuwa safi ya kupikia na kuhamia kwenye Nishati safi ya kupikia.


Dkt. Biteko ametoa rai hiyo leo mkoani Rukwa wakati wa kuweka Jiwe la msingi la mradi wa kusafirishia umeme kilovoti 400 kutoka mkoani Iringa,Mbeya na Sumbawanga(Rukwa) hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya kata ya Malangali. Mradi huo utagharimu Shilingi bilioni 517.




‘’Tutaangalia namna ya kupata fedha kwajili ya kuongeza Mfuko wa Nishati safi ya kupikia ili Watanzania waweze kupata Nishati safi ya kupikia’’ amesema Dkt. Biteko.

Naye Balozi wa Mtu Ni Afya, Mrisho Mpoto amesema anaiomba jamii ifanye kweli katika kutumia nishati safi ya kupikia na wasibaki nyuma. Amesema ni wakati sasa watu waachane na Nishati isiyokuwa safi katika kupikia.

Na Mwandishi Wetu, Rukwa
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)