BIL.22 KUJENGA SOKO NA STENDI USHIROMBO, BUKOMBE

KADUSHI MEDIA
By -
0

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema serikali imetenga shilingi bilioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa soko na stendi ya mabasi ya kisasa katika eneo la Ushirombo Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.

Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 15.8 zitatumika katika ujenzi wa soko jipya la kisasa na Sh bilioni 6.26 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa stendi ambapo Serikali imetoa Sh bilioni 1 kama malipo ya awali ya utekelezani wa miradi hiyo inatarajia kuanza katika mwaka wa fedha 2024/25.



Akizungumza na wananchi wa Ushirombo leo Julai 28 ,2024 mkoani Geita, Mhe.Katimba amesema ujenzi wa somo hilo unaenda sambamba na mahitaji ya kipindi cha sasa.

Amesema soko la sasa uwezo wake vibanda vinavyoweza kubeba wafanyabishara 734 ambapo wenye vibanda halali ni 534 na wasio na vibanda ni 200.

Katimba amesema kuwa Serikali inawekeza Sh bilioni 15.89 kwenye ujenzi wa soko la kisasa litakalokuwa na mabanda kwa ajili ya kutosheleza wafanyabiashara 1,301.

"Ndugu zangu hii ni baraka kubwa sana kwa kuwa uwezo wa soko utaongezeka, wafanyabiashara wenye vibanda ambao kwa sasa wako 534 lakini soko likiboreshwa wataongezeka hadi kufikia wafanyabiashara 1,301."




Amesema kuwa uwekezaji huo mkubwa si kuwa utawanufaisha wafanyabiashara bali litasaidia kupata maeneo mazuri yakufanyia biashara inayokidhi kupata mitaji kwa wakati.

Katimba amesema kuwa kupitia ujenzi huo wa soko la kisasa utasaidia ongezeko la mapato katika halmashauri ambapo awali halmashauri ilikuwa ikikusanya kiasi cha Sh milioni 51.3 kwa mwaka lakini soko likijengwa mapato yataongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 2.2 kwa mwaka.

Amesema kwa upande wa mradi wa stendi eneo le Ushirombo Katimba amesema kuwa kwa sasa stendi hiyo ina uwezo wa kupokea mabasi 50 kwa siku lakini baada ya kujengwa itakuwa na uwezo wa kupokea mabasi yasiyopungua 210 kwa siku.

Amesema pia ongezeko la mapato ni kutoka Sh milioni 155 kwa mwaka hadi kufikia Sh bilioni 1.4 kwa mwaka.

"Haya ni maendeleo makubwa yanayoenda kutokea ambayo yatasaidia kuboresha mapato ya halmashauri na jamii kwa ujumla ambapo yatasaidia kuboresha masuala mbal





Na Mwandishi wetu Geita

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)