WATUHUMIWA WA MAUAWAJI YA MTOTO ASIMWE WAKAMATWA

KADUSHI MEDIA
By -
0


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema tayari Jeshi la Polisi, limewakamata wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mtoto Asimwe Novath (2) mwenye ualbino. Mwili wa Asimwe umepatikana jana ukiwa katika mfuko wa sandarusi, huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa.



Ikumbukwe Mtoto Asimwe alichukuliwa na watu wasiojulikana nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera, Mei 30, 2024 na juhudi za kumtafuta hazikuzaa matunda hadi hapo jana ulipopatikana mwili wake.Hata hivyo, tayari mtoto huyo ameshazikwa leo nyumbani kwao Muleba.
Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na vidhibiti vya kutenda kosa hilo"Sio kwamba tumebahatisha labda tumekamata tu mtu tunadhani hapana, hawa wamepatikana na vidhibiti," amesema.Waziri Masauni ameeleza hayo leo Jumanne, Juni 18, 2024 wakati akizungumza na Mwananchi Digital.


Aidha Alipoulizwa idadi yao, hakuwa tayari kubainisha kwa kile alichofafanua tayari ameshalielekeza Jeshi la Polisi litoe taarifa hiyo na kwamba litaitoa hivi karibuni. "Hakuna hata mtu mmoja ambaye alihusika na huu udhalimu kwa mtoto malaika wa Mungu atakayepona, tumefikia pazuri," amesema.

Ameongeza "Hata hivyo, amesema kilichofanyika kinapaswa kuwa fundisho kwa wahalifu wengine.Tupo vizuri katika kukabiliana na uhalifu na ndiyo maana hakuna mtu atakayefanya uhalifu asipatikane," amesema Masauni.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)