RC MTANDA AWATAKA WANA BUCHOSA KUMUENZI SHINDIKA KWA MAZURI ALIYOYAFANYA

KADUSHI MEDIA
By -
0

 


Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo mei 18, 2024 amewaongoza wananchi wa Buchosa na Wilaya ya Sengerema kiujumla katika kumuaga na kisha ibada ya mazishi ya aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Timothy Bukombe Shindika aliyefariki Mei 14, nyumbani kwake Wilayani Sengerema.


Wakati akitoa salamu za Mkoa Mhe. Mtanda ametoa rai kwa wanafamilia ya marehemu Shindika, wananchi wa Buchosa na Wilaya ya Sengerema kuendelea kumuenzi marehemu Shindika kwa mazuri aliyoyafanya ndani ya Serikali na ndani ya kanisa lakini pia kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili ampokee na kumuweka mahala pema peponi.


Aidha, RC Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza bado ulikuwa una uhitaji wa busara na hekima za Mzee Shindika lakini mipango ya Mungu haizuiliki.

"Sisi watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa tumepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa sana, mzee wetu alikuwa ana umri mkubwa sana lakini bado alikiwa ni hazina kubwa kwa nchi yetu lakini pia hazina kwa kanisa na kwa familia".

Marehemu Timothy Shindika amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanzakwa mwaka 1987 -1992.





Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)