RC MTANDA AWAPA SIKU SABA TAMESA KUPELEKA KIVUKO KISORYA - UKEREWE

KADUSHI MEDIA
By -
0


 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa siku saba kwa Wakala wa Ufundi na Umeme, TAMESA kuleta Kivuko kutoka Sengerema kuja kuvusha abiria wa Kisorya kwenda Ukerewe baada ya kushuhudia ubovu wa Mv Ujenzi.


Mtanda akiwa njiani leo kuelekea Ukerewe kuhudhuria Maadhimisho ya siku ya Familia Duniani, akizungumza na abiria hao amesema ni lazima kuwepo na vivuko viwili ili kuepusha kuwacheleweshea shughuli zao wananchi huku kikisubiriwa kuja rasmi Kivuko kipya.


"Nimeona hali ya kusua sua kwa kivuko cha MV Ujenzi ikiwemo Injini kuzima nimeambiwa kina tatizo la Injini kuingia maji, sasa nawaagiza TAMESA wafike haraka leo hapa kurekebisha changamoto hii, hili siyo tatizo kubwa la kuwatesa wananchi," amesisitiza Mhe. Mtanda.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali imegharamia Milioni 892 kivuko kipya kitakachoanza kuvusha abiria eneo la Kisorya-Rugenzi na atahakikisha kinakamilika haraka ili kurahisisha huduma za wananchi.

Akiwa kwenye mkutano mfupi na watumishi wa Halmashauri ya Ukerewe, Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha kutoa huduma bora kwa wananchi hali ambayo watafanya waipende Serikali yao.

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ndubiagai ameishukuru Serikali kwa kuleta miradi mbambali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

"Tumepatiwa zaidi ya Shs. Bilioni 1 ya ujenzi wa jengo la Utawala "Mkuu wa Wilaya.

BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO






Na Pascal Kadushi
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)