Rai hiyo imetolewa leo Aprili 23, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala wakati akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye wa uzinduzi wa kampeni ya elimu kwa umma kanda ya ziwa kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa minara 758 nchini.
“Naupongeza Mfuko wa UCSAF kwa lengo zuri la kuzindua mpango huu, serikali yetu imeonesha dhamira kwa vitendo mkakati wa kumletea maendeleo mwananchi hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha inakuwa na tija." Mkuu wa Wilaya.
Vilevile, amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwezesha miradi mbalimbali hususani katika miradi ya mawasiliani ambayo itaenda kusaidia umma kwenye kurahisisha shughuli za kiuchumi.
Naye Afisa Mawasiliano wa UCSAF Celina Mwakabwale amesema wanafikisha huduma za mawasiliano katika maeneo mengi yaliopo vijijini na machache yaliyopo mjini ambapo mnara mmoja unagharimu milioni 300 mpaka 350.
“UCSAF kwa kutambua umuhimu wa mawasiliano inashirikiana na makampuni ya simu kama Vodacom,Airtel,halotel,TTCL na mengine kuwapa ruzuku ili kujenga miradi ya minara”Mwakabwale
Meneja wa Mfuko huo Kanda ya ziwa Mhandisi Benard Buremo aliyetoa taarifa kwa kina kuhusiana na miradi hiyo amebainisha huduma ya mawasiliano kuanzia vijijini inakwenda vizuri ambayo ndiyo malengo ya Serikali
Kwa upande wake Afisa Tarafa kutoka Mumbuga Ukerewe, Josephat Mazula amesema Serikali inatakiwa kuboresha minara ambayo tayari inafanya kazi ambayo kazi zake zimekuwa hafifu wanatakiwa kuhakikisha mawasiliano yanakuwa ya uhakika.
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi huo walikuwa Makatibu Tawala,Watendaji wa kata, na Wakuu wa Wilaya.
Baadhi ya Picha za tukio la uzinduzi wa kampeni ya elimu kwa umma kanda ya ziwa
Na Pascal Kadushi
Kwa msaada wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza