MTU mzima mmoja kati ya wanne bado hulala taa zikiwa wazi huku wengine wakikimbia kunapokuwa na giza, utafiti umeonyesha.
Kulingana na wanasayansi, kati ya watu wazima zaidi ya 2,000, nusu yao bado huogopa giza.
Wanasaikolojia wanasema kuwa uoga huu ni ishara kuwa mtoto mdogo anayekuwa ndani ya kila mtu husalia na mtu maisha yake yote.
Kwa upande mwingine pia, uoga huu ni ishara kuwa hofu na wasiwasi ambao mtu alikuwa nao akiwa mtoto unajionyesha baadaye maishani.
Hofu ya giza ni kawaida utotoni lakini hupungua kadri umri unavyoongezeka wanapogundua kwamba ingawa inaweza kuwa giza, hawako peke yao, na watu wao wanaowajali hawajatoweka.
Hali kadhalika, watu wazima nao huhusisha giza na kutokuwa na uwezo wa kudhibiti mambo huku wakifikiria kuwa ikiwa hawawezi kuona, wanaweza kuogopa mambo mabaya yawatendekee usiku.