Wangaza wa simu hutatiza uzalishaji wa 'melatonin', homoni ambazo hudhibiti mzunguko wa mwili kulala. Sio tu kusababisha ukosefu wa usingizi na uchovu, lakini pia huweza kusababisha madhara kadhaa ya afya ukiwamo ugonjwa wa moyo, uzito mwingi, msongo wa mawazo, na wasiwasi.
Homoni aina ya 'melatonin' hupambana na seli hatari ambazo husababiasha saratani, hivyo basi ikiwa homoni hizo hazitazalishwa kwa viwango vinavyostahili, utakuwa katika hatari ya kupata kansa na maradhi mengine ya macho.